Moto wawaka, wanachuo wakiwa ibadani

Ibada ya kusifu na kuabudu USCF. 


USCF, ni moja ya kanisa linalopatikana katika chuo kikuu cha dodoma katika ndaki ya hinsia na sayansi ya jamiii kwa kiingereza ikijulikana kama humanity and social science. Pia inajumuisha baadhi ya wanafunzi wanaotoka katika shule zingine kama COBE na SOlo.

Hii ni moja kati ya ibada ambayo ilifanyika katika kanisa hilo ikifahamika kama "nusu mkesha" kwa ajili ya kumshukiru MUNGU wakati wakiwa wanajiandaa kuelekea kumaliza masomo ya muhura wa kwanza mwaka 2023. Ibada hiyo ilianza majira ya saa mbili na nusu usiku na kutamatika saa saba usiku. Pia ilikuw na wangeni waarikwa mbalimbali ambao walihudumu katika ibada hiyo mpaka mwisho.

"Mbali na masomo na mambo mengine ya kitaaluma lakini lazima tumwabudu MUNGU na kumsifu katika viwango vikubwa" ayo ni maneno ya mwimbaji anayejulikana kama JACKLIN, aliyehudumu katika uimbaji kama mgeni mwalikwa kwenye ibada hiyo. MUNGU wetu ni mwaminifu sana sana na zaidi hawezi kukuacha katika kitu chochote ukimtumikia, kwahyo lazima tumtumikie yeye Leo na hata milele za maisha yetu.

Kuhusu ibada hiyo, watu walisifu , waliabudu, waliimba katika viwango vikubwa kadri vile roho wa MUNGU alivyowasaidia na kuwatumia. Pia zaidi wanavipaji vya kupiga kila aina ya kifaa cha mziki kama vile kinanda, gitaa, drums na filimbi. Yote hayo ufanyika katika weredi mkubwa sana maana chuo hicho Cha UDOM kinajumuisha watu kutoka sehem mbalimbali.

Pia neno la MUNGU linahubiriwa sana sana zaidi na kusaidia watu kumjuwa MUUMBA wao siku zote za maisha yao. Kupitia mchungaji mlezi wa USCF ambaye ndie anayeusika kusimamia malezi ya vijana wote wanaotoka katika makanisa yaliyo chini ya CCT na kuunda umoja unaojulikana kama USCF, ndie anayeratibu shughuri zote za mpangilio wa utoaji wa neno la MUNGU yaani mahubiri katika makanisa yote ya USCF yaliopo chuoni hapo. pia n mtu ambaye anapenda kazi yake pamoja na kupenda vijana wake kadri ROHO wa MUNGU anavyomtumia.

Chuoni kuna mambo mengi yanayotokea, yanayopelekewa na uwepo wa changamoto za kimaisha na uhaba wa fedha. Hali inayopelekea wanafunzi wengi kushindwa kuendelea na masomo yao, hvyo wanamwitaji MUNGU na msaada wake ili waweze kuwa salama kabisa kitaaluma, kimaisha na kuwa na amani mioyoni mwao. Maana bila MUNGU amna lolote wanaliweza kufanya katika maisha yao likasimama imara zaidi bila tatzo.

Tembelea BUSHIRI TV ONLINE, ili kuona namna ambavyo watumishi waliopo vyuoni wakiwa wanamtumikia MUNGU Kwa viwango vikubwa sana.

Maoni