UDOM panukia hatari

Chuo kikuu cha dodoma kinachofahamika kama UDOM, kipo kwenye maandalizi mazito ya kuelekea kwenye mitihani ya kumaliza muhura wake wa pili unaojulikana kama second semester (ii). kupitia mitihani yake ya mwisho wa muhura yaani university examination (UE).

Kupitia vyanzo mbalimbali imefahamika kuwa mitihani hiyo itaanza kutimua vumbi rasmi kuanzia tarehe 28/6/2023 na inatazamiwa mitihani hiyo kuisha tarehe 14/7/2023. Kwa ujumla mitihani hiyo itafanyika takribani wiki 3. Huku Wanafunzi mbalimbali wakizidi kutoa maoni yao kuhusiana na ratiba hii ya mitihani iliyoko mbele yao.

" Tumejiandaa vizur na tunapokea katika hicho la tatu mitihani hii pamoja na ratiba yake ambayo mpaka sasa tumepewa second draft, na tupo tayari kushiriki na kuifanya katika mazingira na kiwango bora zaidi, kikubwa ni kuwa vijana wenzangu tumwombe MUNGU pia tusome kwa bidii zaidi hasa kwa sisi ambao ndio mwaka wetu wa mwisho". Hayo ni maneno ya mwanafunzi anayejulikana kwa jina la BUSHIRI.

UDOM, ina jumla ya shule 7 yaaan CHSS,COBE,CIVE,TIBA,COESE,COED na CBSL ambazo kwa pamoja zitahusika kwenye kufanya mitihani hiyo ya kumaliza mwaka huu isipokuwa TIBA;ambayo yenyewe ratiba zake zinatofautiana na shule ama taasisi zingine zinazounda kwa ujumla UDOM,


Maoni

Chapisha Maoni